1. Biismillahi Jalali
Biismillahi Awali
Biismi natawakali
Kwa jina lake Jaliya.
2. Thumma ninamswalia
Kipenzi chetu nabia
Na alize wote pia
Na Isilamu jamiya.
3. Nataka kutafakari
Juu ya hii bandari
Niangalie mazuri
Na atharize pamoya.
4. Bandari hii ya Lamu
Mji wa waisilamu
Mji ulositaqimu
Mila na muruwa piya.
5. Lakini watu hunena
Ni mji wa nyuma sana
Maendeleo hakuna
Ni haba mno sikiya.
6. Waswahili watwambia
Na sote tumesikia
Mgeni akiwajia
Wenyeji hujiponeya.
7. Bandari imetujia
Ni mgeni wetu pia
Yapasa kufurahia
Kwa shangwe kumpokeya.
8. Mgeni hakuja pweke
Unayo mizigo yake
Zawadi kutoka kwake
Sisi ametueteya.
Biismi natawakali
Kwa jina lake Jaliya.
2. Thumma ninamswalia
Kipenzi chetu nabia
Na alize wote pia
Na Isilamu jamiya.
3. Nataka kutafakari
Juu ya hii bandari
Niangalie mazuri
Na atharize pamoya.
4. Bandari hii ya Lamu
Mji wa waisilamu
Mji ulositaqimu
Mila na muruwa piya.
5. Lakini watu hunena
Ni mji wa nyuma sana
Maendeleo hakuna
Ni haba mno sikiya.
6. Waswahili watwambia
Na sote tumesikia
Mgeni akiwajia
Wenyeji hujiponeya.
7. Bandari imetujia
Ni mgeni wetu pia
Yapasa kufurahia
Kwa shangwe kumpokeya.
8. Mgeni hakuja pweke
Unayo mizigo yake
Zawadi kutoka kwake
Sisi ametueteya.
9. Tujue huyu mgeni
Takaa nasi jamani
Muda mrefu yaqini
Zawadi kitupatiya.
10. Zawadi moja muhimu
Ni ilee ya ilimu
Watu wengi kwetu Lamu
Elimu kujipatiya.
11. Leo twaona vijana
Kusoma wahimizana
Na mawazo kupeana
Masomo kuendeleya.
12. Na pia nina imani
Bandari itadhamini
Vijana wende vyuoni
Taaluma kusomeya.
13. Natija yake ni kuwa
Taaluma tutajuwa
Nyadhifa tutatukuwa
Mambo yetu kwendesheya.
14. Ni ufunguo elimu
Hutatua kila gumu
La binafsi na qaumu
Mengi yatatunyokeya.
15. Kazi nyingi zitakuya
Watu watajipatiya
Nyengine zitabakiya
Wengine kujishindiya.
Takaa nasi jamani
Muda mrefu yaqini
Zawadi kitupatiya.
10. Zawadi moja muhimu
Ni ilee ya ilimu
Watu wengi kwetu Lamu
Elimu kujipatiya.
11. Leo twaona vijana
Kusoma wahimizana
Na mawazo kupeana
Masomo kuendeleya.
12. Na pia nina imani
Bandari itadhamini
Vijana wende vyuoni
Taaluma kusomeya.
13. Natija yake ni kuwa
Taaluma tutajuwa
Nyadhifa tutatukuwa
Mambo yetu kwendesheya.
14. Ni ufunguo elimu
Hutatua kila gumu
La binafsi na qaumu
Mengi yatatunyokeya.
15. Kazi nyingi zitakuya
Watu watajipatiya
Nyengine zitabakiya
Wengine kujishindiya.
16. Kazi aina aina
Takuwa zapatikana
Kwa waliosoma sana
Na wasosoma pamoya.
17. Kwa kazi kujipatiya
Maisha yatatengeya
Mahitaji kuqidhiya
Ufuqara kupoteya.
18. Lamu sana itang’ara
Zitanyoka barabara
Kurahisisha safara
Za ndege na reli piya.
19. Biashara zitangiya
Na bidhaa zitakuya
Huduma kujipatiya
Kwa rahisi nakwambiya.
20. Uongozi kwa hakika
Nao utaimarika
Watu watawajibika
kuchagua wanofaa.
21. Watu watawachaguwa
Viongozi wa muruwa
Kazi wanaoijuwa
Jamii kuendesheya.
22. Uongozi ulobora
Ndio jamii imara
Lamu naipa bishara
Takuwa bora sikiya.
Takuwa zapatikana
Kwa waliosoma sana
Na wasosoma pamoya.
17. Kwa kazi kujipatiya
Maisha yatatengeya
Mahitaji kuqidhiya
Ufuqara kupoteya.
18. Lamu sana itang’ara
Zitanyoka barabara
Kurahisisha safara
Za ndege na reli piya.
19. Biashara zitangiya
Na bidhaa zitakuya
Huduma kujipatiya
Kwa rahisi nakwambiya.
20. Uongozi kwa hakika
Nao utaimarika
Watu watawajibika
kuchagua wanofaa.
21. Watu watawachaguwa
Viongozi wa muruwa
Kazi wanaoijuwa
Jamii kuendesheya.
22. Uongozi ulobora
Ndio jamii imara
Lamu naipa bishara
Takuwa bora sikiya.
23. Huduma za matibabu
Za maji ziwe karibu
Na taa bila taabu
Takuwa twajipatiya.
24. Teknoloji jamani
Itapanda kama nni
Takua chetu kifani
Uzunguni angaliya.
25. Na miji itafunuka
Na mingine kupanuka
Mashamba yatageuka
Makazi ya kuishiya.
26. Watu wengi watakuya
Wengi sana nakwambiya
Hata milioni moya
Ni ndogo sana sikiya.
27. Watu ni aina mbili
Wazuri na walo dhili
Wazuri twawakubali
Waovu tutayutiya.
28. Usalama tapoteya
amani taizengeya
wasiwasi takungiya
ndiani ukitembeya.
29. Majambazi watazidi
Wizi nao ushitadi
Maa asafi shadidi
Ukahaba taeneya.
Za maji ziwe karibu
Na taa bila taabu
Takuwa twajipatiya.
24. Teknoloji jamani
Itapanda kama nni
Takua chetu kifani
Uzunguni angaliya.
25. Na miji itafunuka
Na mingine kupanuka
Mashamba yatageuka
Makazi ya kuishiya.
26. Watu wengi watakuya
Wengi sana nakwambiya
Hata milioni moya
Ni ndogo sana sikiya.
27. Watu ni aina mbili
Wazuri na walo dhili
Wazuri twawakubali
Waovu tutayutiya.
28. Usalama tapoteya
amani taizengeya
wasiwasi takungiya
ndiani ukitembeya.
29. Majambazi watazidi
Wizi nao ushitadi
Maa asafi shadidi
Ukahaba taeneya.
30. Ardhi zetu za Lamu
Mji wetu mahashumu
Wapewe waso walamu
Watu wageni sikiya.
31. Kuna miji taanguka
Na watu wake kutoka
Bandari itazitaka
Ardhi kuzijengeya.
32. Mazingira tachafuka
Ya mikoko kwa hakika
Samaki kuathirika
Makaziyo kupoteya.
33. Hili litadhuru sana
Uchumi wa tangu jana
Mikoko kukosekana
Na uvuvi kufifiya.
34. Kunayo na yetu dini
Mila na utamaduni
Zitakosa yao shani
Lamu tutazizengeya.
35. Itakosekana dini
watu walewe wazini
si kwa siri, jaharani
na uraibu kweneya.
36. Kweli mgeni akiya
Mwenyeji hufurahiya
Baraka hujipatiya
Kama bandari yo piya.
Mji wetu mahashumu
Wapewe waso walamu
Watu wageni sikiya.
31. Kuna miji taanguka
Na watu wake kutoka
Bandari itazitaka
Ardhi kuzijengeya.
32. Mazingira tachafuka
Ya mikoko kwa hakika
Samaki kuathirika
Makaziyo kupoteya.
33. Hili litadhuru sana
Uchumi wa tangu jana
Mikoko kukosekana
Na uvuvi kufifiya.
34. Kunayo na yetu dini
Mila na utamaduni
Zitakosa yao shani
Lamu tutazizengeya.
35. Itakosekana dini
watu walewe wazini
si kwa siri, jaharani
na uraibu kweneya.
36. Kweli mgeni akiya
Mwenyeji hufurahiya
Baraka hujipatiya
Kama bandari yo piya.
37. Ila mgeni Bandari
Mbali na yake mazuri
Amekuya na athari
Nyengine sikuzitaya.
38. Nitamuomba Jalali
Muweza wa kulla hali
Ayepushe ya thaqili
Ya udhia na baliyya.
39. Yenye kheri ya Bandari
Yaharakishe Jabbari
Yalo na mbovu athari
Yasitwegeme Jaliya.
40. Tupe nguvu tushikane
Yalo mazuri tuone
Hima tusaidiane
Kwenda kuyatapiliya.
41. Maono yangu ni haya
Yalioniafiqiya
Kama nimekosa ndiya
Mngu tanighufiriya.
42. Thumma swala na salamu
Zende kwake muadhamu
Na ali zake kiramu
Na Isilamu jamiya.
Tamat.
Mbali na yake mazuri
Amekuya na athari
Nyengine sikuzitaya.
38. Nitamuomba Jalali
Muweza wa kulla hali
Ayepushe ya thaqili
Ya udhia na baliyya.
39. Yenye kheri ya Bandari
Yaharakishe Jabbari
Yalo na mbovu athari
Yasitwegeme Jaliya.
40. Tupe nguvu tushikane
Yalo mazuri tuone
Hima tusaidiane
Kwenda kuyatapiliya.
41. Maono yangu ni haya
Yalioniafiqiya
Kama nimekosa ndiya
Mngu tanighufiriya.
42. Thumma swala na salamu
Zende kwake muadhamu
Na ali zake kiramu
Na Isilamu jamiya.
Tamat.
(c) Bhaddy Shee.