Ewe usiye na haya
hivi huoni ubaya
kwa kumuasi Jaliya
ilihali mekuleya?
Viumbe wawasitahi
waficha wako wajihi
lakini Mola Ilahi
hata hujamfikiriya.
Watenda yalio mawi
wala khofu huingiwi
na fikira hupitiwi
Mngu akuangaliya
Waiba pia wazini
wasengenya barazani
uwongo na kufitini
ni mambo umezoweya
Tumbo litele haramu
kuswali kwako ni ngumu
wazee huwaheshimu
imekuvaa duniya.
Muonee haya Mngu
si aibu ndugu yangu
wachana na ulimwengu
Allah atakupokeya!
(c) Bhaddy Shee.
No comments:
Post a Comment