"...the more learned a man, the more he see how ignorant he was..."

Wednesday, 9 November 2011

USALAMA JUKUMU LA NANI?


USALAMA JUKUMU LETU

1.       BIISMILLAHI AHADI
KWA INA LAKE WADUDI
ALIFARIDU SWAMADI
INA LAKE NAANDIYA

2.       NIMSWALIYE HABIBU
NIUTIMIZE WAJIBU
NDO NIANDE KUKUTUBU
NUDHUMU KUITUNGIYA

3.       MADA HII KUBWA SANA
NI NDEFU PIA NI PANA
ANIAFIQI RABBANA
YOTE KUIMALIZIYA.

4.       SALAMA NI KUTOKUWA
NA WASI WASI KUNGIWA
UKETIPO KUPUMUWA
MAKINI UMETULIYA.

5.       USALAMA MBWA NAFUSI
USALAMA MBWA UNASI
ALIYE JINI NA NSI
USALAMA HULILIYA.

6.       USALAMA MBWA MUILI
MARADHI KUTOQABILI
USALAMA NI WA MALI
WIZI KUTOKUVAMIYA.

7.       USALAMA WA AKILI
ILIMU SIO JUHALI
NA ULEVI SAMPULI
KUTOPATA KUINGIYA.

8.       NA USALAMA WA HALI
KILA ZAMA NA MAHALI
MTU IWE NI MUHALI
MADHARA KUMTOKEYA.

9.       HAPO ZAMANI ZA KALE
AMU YETU AMU ILE
USALAMA ULITELE
WAZEE WANATWAMBIYA

10.   WATU WALIKIYUWANA
NA WAKIKIRIMIANA
HAKI WAKITUNDIANA
USALAMA UKENEYA.

11.   UTEMBEAPO NDIANI
UKETIPO BARAZANI
UBUKHERI WA AMANI
HAKUNA LAKUTOKEYA.

12.   USALAMA ULOKUWA
MPAKA TWAHADITHIWA
AMU WALIYAMKUWA
MAKA TOTO TWASIKIYA.

13.   YEO SALAMA HAKUNA
NYUMBA HUVUNDWA NTANA
WALEVI WAMEYAZANA
MAJAMBAZI WAMEYAA.

14.   WANENDAPO HARUSINI
WAKE HUSITA ZIDANI
NA ZIPULI NA HERINI
KUNYANG’ANYWA WAHOFIYA.

15.   SUALI NAJIULIZA
HUWAZUA NA KUWAZA
NI NANI ALIYEANZA
MAMBO HAYA KUTWETEYA.

16.   TANENA HAPA SISITI
TWAWAYUWA WAVUNDATI
SIKU ZOTE NI WANATI
NA WAGENI WAKANGIYA.



17.   TUMUATAPO MMOYA
WAWILI WATATU PIYA
NYUNGA WAKITUZANYIYA
NI NNI TWATARAJIYA?

18.   BAROBARO WATANGIYA
KWENYE NYUNGA KUTUMIYA
WAKISINDIA NA NDIYA
NANI MUI TANGALIYA?

19.   TUKIKIRI TEMBO KUYA
BOTI NZIMA KUNGIYA
MADUKA KUZANYA PIYA
MWISHOWE TWAFIKIRIYA?

20.   WALEVI KUTUSUMBUWA
BANATI TUKISHIKIWA
ZIKUMBO TUKIPIJIWA
JEE TWAYATAKA HAYA?

21.   TUWAATAPO WAGENI
WASO KAZI WALA DINI
WALALE VIBARAZANI
MUINI MWETU KUYAA

22.   TAKUWA TWAFUGA WIZI
WALAGHAI MAJAMBAZI
WASO KAZI WALA BAZI
KAZI NI KUTUVAMIYA.

23.   TUSIPOPEKA ZUONI
WANA KUIYUWA DINI
KUTOWAPEKA SHULENI
VIZAZI GANI TWALEYA?

24.   TWALEYA WATU WAZIVU
WASOZITUMIYA NGUVU
WANGOJEA ZILO MBIVU
NAZI KUWAANGUKIYA.



25.   WATAKA WAO WAPEWE
WATAKACHO WAETEWE
WASIPOPATA WENYEWE
UHUNI KUINGILIYA.

26.   TUSILIE NA POLISI
POLISI NI SISI SISI
KULINDA ZETU NAFUSI
NA UMATI WOTE PIYA.

27.   NI LETU SOTE JUKUMU
KUILINDA YETU AMU
MALINDI HATA WATAMU
NA NCHI YOTE PAMOYA.

28.   SOTE TUHIMIZANENI
KUPEKA WANA SHULENI
TUSIKUBALI WAGENI
WASIO PA KWELEKEYA.

29.   TUSIKUBALI WALEVI
WALA WAUZA WALEVI
AMA TUTAFUGA WIVI
LA BUDA NIMEWAMBIYA.

30.   WALE WATU WAUZAO
TEMBO BANGI NYUNGA ZAO
NI ADUI WATU HAO
TUWATOWE MUI PIYA.

31.   TUJITAHIDI TUFANYE
TUPATILIZE PENYENYE
KILIO HULIA MWENYE
NA MTU MBALI KALIYA.

32.   RABBI TUPE USALAMA
UTWENEE SOTE UMMA
DUNIANI NA QUYAMA
WASALAMA NAKOMEYA.
            --TAMAT--

©BHADDY SHEE 14 DHULHIJJAH 1432/ 9.NOV.2011





Tuesday, 1 November 2011

the Flower and the Pearl Analogy...


One day a brilliant beautiful fragrant flower with attractive colours met a Pearl, which lives far in the bottom of the sea and has none of these characteristics. Both got acquainted with each other. The flower said, “Our family is large; roses and daises are members of the family. And there are many other species that are various and countless each has a distinctive scent, appearance etc
Suddenly a tinge of distress appeared on the face of the Flower. “ Nothing accounts for sorrow in your talk. So why are you depressed?  Asked the pearl.
“Human beings deal with us carelessly, they slight us. They don’t grow us for our own good, but to get pleasure from our fragrance and our beautiful appearance. They throw us on the street or in the garbage can after we are dispossessed with the most valuable property; brilliance and fragrance.”
Then the flower sighed. Then it said to the Pearl, “Speak to me about your life. How do you live? How do you feel? You are buried in the deep bottom of the sea.”
The Pearl answered, “Although I have none of your distinctive colors and scent, humans think I am precious. They do the impossible to acquire us. They go on long journeys, dive deep in the seas searching for us. You might be astounded to find that, the farther I we live the more beautiful and brilliant we become. That is what raises up our value, that is what they think. We live in thick dark shell isolated in the dark seas. Nonetheless am happy and proud to live in a safe zone that is far from wanton and mischievous hands and still humans consider us highly valuable.”

Do you realize what the flower and the Pearl symbolize?
Try to think… think… and think…

The flower is the unveiled woman who shows her charms. And the Pearl is the veiled woman who conceals her beauties. I hope that thing will bring to the sisters that don’t wear Hijab the understanding of how precious Muslim women are! And why Allah ordained her to cover her charms. For those sisters that do wear Hijab they should know their value and their worth and keep on with the Hijab, a regalia From Allah!.....