"...the more learned a man, the more he see how ignorant he was..."

Wednesday, 26 June 2013

N'NANI ATABAKIA (MAUT)

Kufa si mtu kuhiti
Kufa pia si bahati
Kufa huwa ni wakati
Wako umekufikiya.

Kufa sife na laiti
Kwa kutenda sayiati
Kufa uwe hasanati
Wende mbee uking'aa

Kufa si lazima nyati
Kukugonga na tiati
Hata mchwa wala miti
Hukuuwa kwa fajaa.

Kufa jaa kizingiti
Hukutoa uhayati
Kukupeka umamati
Ulimwengu mpiyaa.

Kufa hufia umati
Barobaro kwa banati
Wana na maajuzati
Hakuna wa kubakiya.

Kufa hufa miangati
Bamba kofi na boriti
Wewe kitoto kijiti
Hatuwezi kushangaa

Kufa wanakufa nyati
Simba ndovu wenye mati
Faru chui wenye sati
Hunenani wewe paa.

Kufa hufa mwenye noti
Mwenye lulu na yakuti
Kufa hufa fukarati
Basi nani tabakiya?

Tabakiya Jabaruti
Aloumba samawati
Kaitandaza tiati
Mola mpweke taa.

©Bhaddy Shee 2011

No comments:

Post a Comment