"...the more learned a man, the more he see how ignorant he was..."

Wednesday, 26 June 2013

DUA FOR GETTING A GOOD SPOUSE (MUSLIM)

DUA YA KUMRAHISISHIA
MWISLAMU KUPATA MCHUMBA
MWEMA.
***************************************
BISMILLAAHI RRAHMAANI
RRAHIIM. WALHAMDU LILLAAHI
RABBIL `AALAMIIN. WASSALAATU
WASSALAAMU `ALAA ASHRAFIL
MURSALIIN. WA-ALAA AALI
BAYTIHI WASAHBIHI AJMA`IIN.
ALLAAHUMMA INNIY AS-ALUKA
BIANNIY ASH-HADU AN LAA-
ILAAHA ILLA ANTA L-AHADU
SSWAMADU LLADHI LAM YALID
WALAM YUWLAD WALAM YAKUN
LAHU KUFUWAN AHAD. IQDHI
HAAJATIY WA-ANIS WAHDATIY
FARRIJ KURBATIY AJ-`ALLIY
RAFIYQAN SWAALIHAN KAY
NUSABBIHUKA KATHIYRAN
WANADHKURUKA KATHIYRAN FA-
ANTA BIY BASWIYR. YAA
MUJIYBUL MUDHTAR IDHAA
DA`AAK. AHLIL `UQDATI WA-AMIN
RAW`ATIY WAFARRIJ KURBATIY.
YA ILAAHI HABLI MIN LADUNKA
ZAWJAN SWAALIHAN WAJ`AL
BAYNANAL MAWADDATAN
WARAHAMATAN INNAKA `ALAA
KULLI SHAY-IN QADIYR. YAMAN
YAQUWLU LISHAY-IN KUN
FAYAKUWN. ALLAAHUMMA AATINA
FIY DDUNIYA HASANATAN WAFIL
AAKHIRATI HASANATAN WAQINAA
`ADHAABA NNAAR. RABBI LA
TADHARNIY FARDAN WA-ANTA
KHAYRUL WAARITHIYN.

(frm mombasa-toa donge lako)

TAFSIRI YA DUA
..........................................
Kwa jina Mwenye enzi Mngu mwenye kurahamu wema na waovu ulimwenguni na mwenye kurahamu wema watupu kesho akhera.
Kila jinsi ya sifa njema ni zake Mwenye Enzi Mngu mlezi wa viumbe wote. Na swala na amani zimshukie m-bora wa mitume na ahli zake na maswahaba wake.

Ewe mola hakika nakuomba kwa kuwa nashuhudia hapana mola apasaye kuabudia kwa haki isipokuwa wewe mmoja mpweke ambaye hakuzaa wala hakuzaliwa wala hakuna yeyote wa kufanana na yeye.

Niqidhie haja zangu na niondoshee upweke wangu na nifariji dhiki zangu. Nijaalie rafiki ambaye ni mwema ili tukusabih kwa wingi na kukukumbuka kwa wingi hakika wewe kwangu nimuoni (waniona).

Ewe mwenye kumjibu mwenye dhiki anapokuomba. Nifungulie fundo langu ipe amani khofu yangu na niondoshee kero langu.

Ewe Mola nipe na mimi kutoka kwako mchumba mwema na ujaalie baina yetu mapenzi na kuhurumiana hakika ni muweza kwa kila kitu.

Ewe mwenye kusema jambo liwe na huwa. Ewe Mola tupe mema katika dunia na utupe mema akhera na utulinde na adhabu ya moto. Ewe mola usiniache mpweke na wewe ni m-bora wa kurithisha.

Badi. All rights reserved.

1 comment: